Joe Biden: Nitaliunganisha taifa la Marekani

Rais mteule wa Marekani Joseph Robinnete Biden ameapa kuliunganisha taifa hilo huku akiahidi kuponya vidonda vya kisiasa vilivyochipuka wakati wa kampeni.

Katika hotuba yake ya kwanza kama Rais Mteule nyumbani kwake Wilmongton,Delaware, Biden alisema Majimbo mekundu na yale ya Samawati,ni taifa moja la Marekani na atayahudumia bila upendeleo.

Rais huyo mteule, ambaye aliwasili katika jukwaa akivalia barakoa,vile vile alitangaza atabuni kamati ya kukabiliana na virusi vya Covid-19 ili kuhakikisha iko tayari kuidhinisha maamuzi atakayotoa siku ya kuapishwa kwake mwezi Januari mwaka ujao.

Kwa upande wake makamu wa Rais mteule Kamala Harris aliwapongeza raia wa Marekani kwa kumchagua Biden akitaja uchaguzi huo umeleta matumaini makubwa kwa Marekani.

Licha ya kuwa Biden alitangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi huo wa urais,Rais Donald Trump hajazungumza lolote hadhari.

Awali Rais Trump alitaja zoezi la kuhesabu kura kuwa lilighubikwa na udanganyifu.

Trump amewasilisha kesi katika mahakma za majimbo kadhaa kupinga matokeo ya kura za urais, lakini maafisa wa uchaguzi walisema kwamba hakuna ushahidi kwamba kulikuwa na udanganyifu katika uchaguzi huo dhidi yake.

Atakapochukua hatamu za uongozi wa Marekani tarehe 20 mwezi Januari mwaka 2021, Joe Biden atakuwa na umri wa miaka 78 na kuwa rais mkongwe Zaidi katika historia ya Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *