Joe Biden aapishwa kuwa Rais wa 46 wa Marekani

Joe Biden ameapishwa kuwa Rais wa 46 wa Marekani katika sherehe iliyoongozwa na jaji wa Mahakama Kuu John Roberts.

Hata hivyo mtangulizi wake Donald Trump alidinda kuhudhuria Shereha ya kuapishwa kwa Biden na kuingia katika kumbukumbu za historia ya nchi hiyo kuwa rais wa kwanza kutohudhuria sherehe za kuapishwa kwa mrithi wake tangu mwaka 1869.

Punde tu baada ya kuapishwa Biden alitaja siku hiyo kuwa ya kihistoria na iliyojawa matumaini. Alisema ni wakati wa kuwaunganisha wamarekani huku akiahidi kuwahudumia raia wote wa nchi hiyo.

Hafla ya kuapishwa kwa Biden na makamu wake Kamala Harris iliandiliwa chini ya ulinzi mkali huku ikikadiriwa takribani wanajeshi 25,000 walishika doria katika eneo hilo.

Biden aliwashukuru marais wa zamani waliohudhuria hafla hiyo waliojumuisha Barack Obama,Bill Clinton na George W Bush.

Wakati uo huo Rais huyo mpya wa Marekani  alitangaza misururu ya amri inayolenga kugeuza sera kuu za Donald Trump.

Kulikuwa na wasiwasi huenda wafuasi wa Trump wakahujumu shughuli za uapisho hatua iliyosababisha kuwekwa  ulizi mkali.

Waandamanaji wanaomuunga mkono Trump walifanya vurugu tarehe 6 mwezi Januari baada ya Trump kudai kuwa uchaguzi huo ulikumbwa na udanganyifu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *