Joash Onyango awanusuru Simba kutafunwa na Yanga Derby ya Kariakoo

Beki kisiki wa Kenya Joash Onyango aliwanusuru wekundu wa Msimbazi Simba Sports club ,alipoachika bao la dakika ya 86 na kulazimisha Derby ya Kariakoo kuishia sare ya bao 1-1 dhidi ya Young Africans ukipenda YANGA katika pambano la ligi kuu Tanzania Bara VPL ,Jumamosi alasiri katika uchanjaa wa Benjamin Mkapa.

Mashabiki    wa    Simba uwanjani Benjamin Mkapa Jumamosi
Mashabiki wa YANGA uwanjani Benjamin Mkapa Jumamosi

Wenyeji Yanga walitamalaki kipindi cha kwanza huku wakidhihirisha mchezo wa hali ya juu kwa pasi kamilifu na mashambulizi ya uhakika yaliyozaa matunda baada ya  mshambulizi wa kutokea Ghana Michael Sarpong kuwanyanyua mashabiki kwa bao la ufunguzi la dakika ya 32 kupitia mkwaju wa penati iliyotakana na mshambulizi wao kuangushwa na beki wa Simba .

Bao hilo lilidumu hadi mapumzikoni huku mashabiki wa Simba wakilazimika kufyata ndimi kwa muda mrefu uwanjani kutokana na  mashambulizi mengi yaliyoelekezwa katika lango lao.

Hata hivyo kuondolewa uwanjani kwa mshambulizi Sarpong kuliwapa mabeki wa Simba fusra ya kupumua na kupunguza kasi ya Yanga na kosa la dakika ya 86 kutoka

kwa madifenda wa Yanga kukampa Joash Onyango beki kisiki wa Kenya nafasi ya kuirejesha Simba mchezoni huku timu zote zikitoka sare ya bao 1-1 katika derby hiyo na kuzidisha ubabe wa Simba dhidi ya YANGA kwenye Derby hiyo.

Mashabiki zaidi ya elfu 40 waliujaza uwanja wa Benjamin Mkapa hadi pomoni wakivalia jezi za timu zao wakiwa na mirindimo ya nyimbo,magoma na densi uwanjani.

Matokeo hayo yanawaacha Vijana wa jangwani Yanga katika nafasi ya pili kwa pointi 24  kutokana na michuano 10 na ikiwa timu pekee ambayo haijapoteza mchuano katika ligi kuu ya VPL,pointi 1 nyumba ya Azam United fc huku Simba ikishikilia nafasi ya tatu kwa alama 20.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *