Jiji kuu la Tunis lawekewa kafyu kudhiti wimbi la pili la Covid-19

Serikali ya Tunisia imetangaza kafyu katika mji mkuu wa nchi hiyo,Tunis kuthibiti wimbi la pili la maambukizi ya virusi vya Corona.

Hayo yamejiri miezi kadhaa baada ya kulegezwa kwa masharti makali ya awali,ambayo yaliathiri pakubwa uchumi wa nchi hiyo.

Magavana wa majimbo manne yalioko eneo la mji Tunis,wametangaza kupitia runinga ya taifa kwamba kafyu hiyo itaanza saa tatu usiku hadi saa kumi na moja alfajiri kuanzia hivi Alhamisi.

Serikali ya Tunis ilifunga shughuli zote za kiuchumi,ikiwemo mipaka yake mwezi machi mwaka huu kuzuia kusambaa kwa ugonjwa wa Covid-19.

Katika kipindi cha mwezi moja uliopita nchi hiyo imenakili visa vipya zaidi ya elfu-20,hali serikali inasema isipothibitiwa italemaza huduma za afya nchini humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *