Categories
Burudani

Jessica Campbell aaga dunia

Muigizaji huyo ni maarufu kwa majukumu yake kwenye filamu kwa jina “Election” na nyingine iitwayo, “Freaks and Geeks” na ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 38.

Familia yake imetangaza kwamba mwanadada huyo ambaye aliacha kuigiza na kuzamia udaktari wa tiba asilia aliaga dunia tarehe 29 mwezi Disemba mwaka 2020 huko Portland Ore.

Inasemekana kwamba siku hiyo, Jessica alizirai na kuaga dunia akiwa kazini muda mfupi baada ya kuhudumia wagonjwa wake.

Kilichosababisha kifo chake bado hakijabainika.

Campbell alionekana kwenye runinga kwa mara ya kwanza mwaka 1992 kupitia kwa filamu iitwayo ” In the Best Interest of the Children”.

Jukumu kubwa la uigizaji lililofuatia ni lile la “Tammy Metzler’ kwenye filamu kwa jina “Election”. Kwenye Freaks and Geeks, anaigiza kama Amy andrews ambaye ni mchzaji ala ya muziki kwa jina “Tuba” katika bendi ya shule.

Akiwa shuleni humo, anaanza uhusian wa kimapenzi na mvulana anayeitwa Ken jukumu ambalo liliigizwa na Seth Rogen kisha baadaye anamfahamisha kwamba alizaliwa hunta.

Binamu yake Jessica kwa jina Sarah Wessling ameanzisha mpango kwenye mitandao wa kuchangisha pesa za kugharamia mazishi ya Jessica na malezi ya mtoto wake wa kiume wa miaka kumi kwa jina Oliver. Campbell ameacha pia mume kwa jina Daniel, mamake na shangazi yake kati ya wengine wengi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *