Categories
Habari

Jengo la kanisa la JCC Kisumu labomolewa

Jengo lililokuwa likitumiwa na waumini wa Jesus Celebration Centre huko Kisumu limebomolewa,huku serikali ya kaunti inapoendelea kurejesha ardhi ya umma iliokuwa imenyakuliwa.

Kaimu wa meneja wa jiji la Kisumu Abala Wanga alisema kuwa usimamizi wa kanisa hilo ulikuwa umepewa ilani ya kuwataka waondoke kutoka ardhi hiyo.

Maeneo ambayo yatarejeshwa tena chini ya umiliki wa serikali ya kaunti ni pamoja na maegesho ya magari,viwanja vya michezo,bustani na nyumba za baraza la jiji hilo.

Kanisa hilo lilikuwa limejengwa kwenye ardhi iliotengewa ujenzi wa uga wa michezo wa Moi.

Wanga alisema kuwa hawatalegeza juhudi za kurejesha mali ya umma iliokuwa imenyakuliwa na watu bila kujali  vyeo au nyadhifa zao katika jamii.

Aliwataka wale walionyakua ardhi au mali ya umma kinyume cha sheria kuirejesha kwa hiari,la sivyo wapokonywe kwa nguvu na kushitakiwa.

Aidha usimamizi wa jiji la Kisumu umebomoa mabanda yaliokuwa yamejengwa nje ya Chuo cha leba cha Tom Mboya,huku ikisemekana mengine yalikuwa ya waziri wa zamani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *