Janga la Kibinadamu huenda likakumba eneo la Tigray

Vyama vya upinzani katika jimbo la Ethiopia la Tigray,vimeonya kuhusu uwezekano wa kutokea janga la kibinadamu ikiwa misaada haitapelekwa katika sehemu hiyo kwa dharura.

Vyama hivyo vimesema tayari wakazi wa jimbo hilo wanakufa kutokana na njaa na kuitaka jamii ya mataifa kuingilia jambo hilo.

Serikali ya Ethiopia imesema kuwa tayari msaada wa chakula unapelekwa katika sehemu hiyo na kwamba takriban watu milioni 1.5 wameshafikiwa.

Aidha kwa mujibu wa vyama hivyo zaidi ya watu 52,000 wameuawa kwenye mapigno yaliozuka mwezi Novemba mwaka jana.

Hata hivyo havikusema jinsi vilivyochakata takwimu hizo,japo duru hizo zilisema waliofariki kwenye mtafaruku huo ni pamoja na wanawake,watoto na viongozi wa kidini.

Serikali ya Ethiopia haijatoa takwimu zozote kuhusu athari za mapigano hayo na badala yake kusema kwamba majeshi yake yanapigana na waasi wa chama cha ukombozi wa jimbo la Tigray-TPLF ambao walitwaa vituo kadhaa vya kijeshi kufwatia kuchachuka kwa uhusiano kati ya utawala wa jimbo hilo na serikali kuu ya waziri kuu Abiy Ahmed.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *