Jamii ya Maasai yasema inaunga mkono ripoti ya BBI

Jamii ya Maasai imesema itaunga mkono mpango wa maridhiano wa BBI ukitaja mapendekezo yaliyomo kuwa yatasuluhisha matatizo yanayokumba jamii hiyo.

Ikiongozwa na mwanaharakati wa ardhi Prof Meitamei Olol Dapash,viongozi wa jamii hiyo walielezea imani yao kwamba dhuluma za ardhi zilizowaathiri kwa muda mrefu zitatatuliwa.

Kulingana na mwanaharakati huyo, ujumuishaji wa hazina ya maendeleo ya uwakilishi wadi, utawawezesha wanachama wa mabunge ya kaunti kutekeleza majukumu yao vilivyo.

Dapush alitoa wito kwa Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga kuhakikisha maoni ya jamii hiyo yaliyokabidhiwa jopo la BBI yanajumuishwa.

Kwa upande wake mwakilishi wadi ya Siana Dominic Rakwa alisema wanasuburi ripoti hiyo iwasilishwe katika bunge la kaunti akiongeza kuwa tayari wameshinikiza uungwaji mkono wa ripoti hiyo.

Mkaazi mmoja Ken Nkamasiai aliunga mkono pendekezo la kuongeza maeneo bunge akisema itahakikisha uwakilishi bora na kuimarisha utoaji huduma kwa wananchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *