Jambojet kuwatuza zaidi ya wateja 1000 kwa kuwapunguzia nauli

Shirika la huduma za ndege la gharama nafuu la Jambojet limeshirikiana na kampuni ya teknolojia ya Cellulant katika kuwatuza zaidi ya wateja elfu-1 vocha za kuwapunguzia nauli.

Ushirikiano huo na kampuni ya Cellulant ambayo inagharamia malipo ya kwenda pekee, ni sehemu ya juhudi zinazoendelea za kuhimiza safari za humu nchini katika kipindi hiki cha kawaida mpya.

Msimamizi wa mauzo wa shirika la Jambojet, Titus Oboogi alisema vocha hizo zitawawezesha wateja kuokoa pesa katika gharama zao za uchukuzi huku sekta hiyo ikijitahidi kujinusuru kutokana na athari za ugonjwa wa COVID-19.

Shirika la Jambojet limerejelea shughuli zake za usafiri wa humu nchini hasa kutoka Nairobi kwenda Mombasa, Eldoret, Kisumu, Malindi na Ukunda(Diani).

Shirika hilo la ndege pia lilizindua safari za moja kwa moja kutoka Mombasa kwenda Eldoret na Kisumu, na vile vile huduma za ukodishaji ndege kuambatana na malengo yao ya maendeleo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *