Jaji Martha Koome naye asailiwa katika wadhifa wa Jaji Mkuu

Juhudi za kumtafuta Jaji Mkuu mpya zimeingia siku ya tatu leo huku Jaji Martha Koome akiwa anaendelea kusailiwa.

Jaji Koome, ambaye kwa sasa anahudumu katika Mahakama ya Rufaa Jijini Nairobi, anahojiwa na jopo la majaji tisa chini ya uenyekiti wa Profesa Olive Mugenda.

Jana ilikuwa fursa ya Profesa Patricia Mbote, aliyesema ana matumaini kwamba kesi zote za kupinga matokeo ya uchaguzi zinapaswa kumalizikia katika mahakama za rufani, na wala sio kupelekwa katika Mahakama ya Juu.

Profesa Mbote anasema wakati wa uchaguzi, ni muhimu kuhakikisha kwamba pande husika zinasuluhisha tofauti zao bila kuelekea kwenye mahakama ya juu.

Akiongea wakati wa kusailiwa kwake mbele ya Jopo la Tume ya Huduma za Idara ya Mahakama, Profesa Mbote alisema kesi zinapaswa kumalizika, hususan kama zimewekewa muda maalum.

Kuna watahiniwa 10 ambao wamependekezwa kwa wadhifa wa Jaji Mkuu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *