Italia yafunga shughuli zote za kiuchumi kwa siku tatu kudhibiti Covid-19

Italia imetangaza kipindi cha siku tatu cha kufungwa kwa shughuli zote za kiuchumi katika juhudi za kuzuia msambao wa uonjwa wa Covid-19 msimu huu wa pasaka.

Hatua hiyo inahusisha mikoa yote huku taifa hilo likipambana na wimbi la tatu la maambukizi ya corona – ambapo karibu visa elfu-20 vinaripotiwa kila siku.

Safari zozote zisizo za muhimu zimepigwa marufuku, lakini watu wameruhusiwa kuwakaribisha hadi watu wawili nyumbani kwao ili kusherehekea pasaka kwa pamoja.

Aidha, makanisa hayajafungwa lakini waumini, wameambiwa kuhudhuria ibada katika maeneo yao.

Kwa mwaka wa pili, Baba mtakatifu Francis atatoa ujumbe wake wa Pasaka pasipo watu katika uwanja wa St Peter’s Square.

Uamuzi huo wa Italia unajiri wakati ambapo nchi kadhaa za bara Ulaya zinajaribu kudhibiti ongezeko la visa vya maambukizi ya corona, huku mipango ya uzinduzi wa chanjo ikiwa imecheleweshwa.

Kwa ujumla, zaidi ya watu 110,328 wamefariki nchini Italia kutokana na janga la corona, huku visa 3,629,000 vya maambukizi ya ugonjwa huo vikiwa vimethibitishwa kufikia sasa .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *