Israeli yasambaza dozi 5,000 za chanjo ya corona kwa wahudumu wa afya wa Palestina

Israeli inasema imepeleka dozi elfu tano za chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 kuwachanja wahudumu wa afya wa Wapalestina, ambao wako katika mstari wa mbele.

Israeli ina mojawapo wa mipango bora zaidi ya chanjo duniani, lakini Wapalestina katika eneo inalokalia la ukingo wa Magharibi ya Mto Jordan na ukanda wa Gaza, hawajapokea chanjo.

Huku wataalamu wa Umoja wa Mataifa wakisema Israeli ina wajibu wa kuwapelekea chanjo Wapalestina, Israeli inasema hiyo si sehemu ya itifaki zilizoafikiwa, na haijapokea ombi kutoka kwa wapalestina.

Huku ikiwa na mkataba maalumu na kampuni ya kutengeneza chanjo ya Pfizer, Israeli imewachanja watu wengi zaidi kuliko nchi nyingine yoyote.

Watu milioni 1.7, ambao ni karibu asilimia 20 ya idadi ya watu, tayari wamepokea chanjo zote mbili, huku zaidi ya watu milioni tatu wakipokea chanjo ya kwanza.

Hata hivyo, kafyu ingali inatekelezwa nchini humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *