Ismail Omar Guelleh achaguliwa bila kupingwa kuiongoza Djibouti

Kiongozi mkongwe wa Djibouti Ismail Omar Guelleh alichaguliwa tena kuwa rais kwa muhula wa tano kwa zaidi ya asilimia 98 ya kura zilizopigwa.

Hata hivyo uchaguzi huo ulisusiwa na upinzani.

Raia wapatao 215,000 walisajiliwa kupiga kura kwenye kinyanganyiro kati ya Guelleh mwenye umri wa miaka 73 na mfanyibiashara asiyejulikana ambaye hakuonekena kuwa tisho kwa kiongozi huyo ambaye amekuwa mamlakani tangu mwaka wa 1999.

Shughuli ya kuhesabu kura ilianza muda mfupi baada ya kufungwa vituo vya kupigia kura saa moja usiku katika taifa hilo la upembe wa Afrika ambalo liko katika eneo muhimu la kibiashara kati ya bara Afrika na rasi ya mataifa ya kiarabu.

Waangalizi wa uchaguzi walisema uchaguzi huo uliandaliwa kwa njia shwari.

Awali baada ya kupiga kura katika mji mkuu ambako wakazi wengi wa raia milioni moja wa Djibouti wanaishi, Guelleh alipongeza jinsi uchaguzi huo ulivyoandaliwa kwa njia shwari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *