Iran yataka Umoja wa Mataifa kulaani mauaji ya Mohsen Fakhri-Zadeh

Iran imelitaka baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kukashifu mauaji ya mtafiti mkuu wa Kinuklia nchini humo Mohsen Fakhri-Zadeh na kuwaadhibu waliotekeleza kitendo hicho.

Hata hivyo wito huo wa Iran kulingana na maafisa wa ubalozi huenda ukapuuzwa.

Baraza hilo la usalama lenye mataifa yanachama 15 huenda siku ya Ijumaa likajadilia faraghani mauaji ya mwanasayansi Mohsen Fakhri-Zadeh.

Hata hivyo mjadala huo utafanyika iwapo mwanachama yeyote ataomba mkutano kama huo ufanywe au wanachama wa baraza hilo wakubaliane kuhusu suala hilo.

Lakini mwakilishi wa Afrika Kusini katika baraza la umoja wa mataifa, Jerry Matjila, amesema hakuna mwanachama yeyote aliyeomba kuandaliwa kwa mkutano wa kujadilia mauaji hayo.

Mabalozi pia wamesema hakujakuwa na majadiliano yoyote kuhusu taarifa hiyo.

Mtafiti huyo aliuawa karibu na Jiji kuu Tehran huku akizikwa kijeshi na serikali ya nchi hiyo.

Hadi sasa hakuna nchi ambayo imedai kutekeleza mauaji hayo licha ya kuwa Iran inailaumu Israeli.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *