IPOA yataka vituo vya Polisi kuwa na vyumba vya kuwatenga wagonjwa wa Covid-19

Halmashauri huru ya kutathimini utendakazi wa maafisa wa polisi-IPOA imehimiza serikali kubuni vyumba vya kimatibabu vya kuwatenga wagonjwa wa COVID-19 kwenye seli za polisi na magereza ili kudhibiti msambao wa ugonjwa huo.

Akiongea wakati wa ziara ya maafisa wa halmashauri ya IPOA katika seli za polisi huko Busia kukadiria mikakati iliyowekwa kuwalinda mahabusu na maafisa wa polisi dhidi ya maambukizi ya Corona, kamishna wa IPOA, Walter Owen alisema ipo haja ya kubuni vyumba vya kuwatenga waathiriwa endapo kutatokea chamuko la COVIDI-19 kwenye magereza na seli za polisi.

Owen alipongeza serikali kwa kubuni seli tofauti za watoto, wanawake na wanaume lakini akatilia mkazo uzingatiaji wa kanuni zilizowekwa na wizara ya afya.

Aidha, halmashauri ya IPOA imesema magari yanayotumiwa na polisi kuwapeleka mahabusu mahakamani na magerezani yanapaswa kufukizwa ili kuzuia kuenea kwa virusi vya Korona

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *