India yagundua aina mpya ya Korona isiyoheshimu kinga

Watafiti nchini India wamegundua aina ya virusi vya corona ambayo inaweza kukwepa kinga yoyote katika mwili wa binadamu.

Kikao cha washauri wa maswala ya sayansi kilichobuniwa na serikali ya India kiliwafahamisha maafisa wa utawala kuhusu kujiunda au kujitokeza upya kwa virusi hivyo vya korona katika baadhi ya Sampuli.

Hata hivyo, washauri hao walisema kuwa hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kuhusiana na hali hiyo.

Kikao hicho cha washauri ambacho kinafahamika kama ‘The Indian SARS-CoV-2 Genetics Consortium’, kimegundua kujitokeza upya kwa virusi hivyo hali ambayo kinaamini kuwa inapaswa kudhibitiwa.

Wanasayansi pia wanachunguza kile kilichosababisha kuongezeka kwa visa vya maambukizi nchini India.

Shirika la Afya Duniani (WHO) halijatangaza aina hiyo ya virusi inayopatikana nchini India kuwa hatari kama lilivyofanya katika mataifa ya Uingereza, Brazil na Afrika kusini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *