IEBC yawataka wanasiasa kuhitimisha kampeni huku chaguzi ndogo kadhaa zikiandaliwa Alhamisi

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini IEBC imewaonya wanasiasa dhidi ya kuendeleza kampeni baada ya kukamilika rasmi kwa muda wa kampeni.

Kupitia kitandazi chake cha Twitter, tume hiyo imesema muda rasmi wa kampeni za chaguzi ndogo za Kaunti ya Machakos na maeneo bunge ya Kabuchai na Matungu utakamilika leo.

Hali ni hiyo hiyo katika wadi kadhaa ambazo pia zitandaa chaguzi ndogo tarehe 4 mezi huu.

Pia tume hiyo imesema shughuli ya kuwahamasisha wapiga kura inaendelea ili kuwawezesha kuelewa utaratibu wa kura, umuhimu wa kushiriki na kufanya maamuzi yafaayo.

Maafisa wa usalama pia wanapokea maelezo kuhusu kusimamia chaguzi hizo ndogo.

Huko Machakos, kiti cha seneta kiliachwa wazi kufuatia kifo cha Seneta Boniface Kabaka ilahali viti vya ubunge vya Matungu na Kabuchai vilibaki wazi kufuatia kufariki kwa wabunge Justus Murunga na James Lusweti Mukwe mwaka jana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *