IEBC yataka kutengewa pesa kabla ya kuthibitisha saini za kuunga mkono BBI

Tume huru ya uchaguzi na mipaka  inataka wizara ya fedha kuandaa  bajeti kabla ya kuchukua hatua ya kuthibitisha saini zilizokusanywa za kuunga mkono mpango wa maridhiano wa  BBI.

Akiongea kwenye afisi za tume hiyo baada ya kupokea saini millioni 4.4  na nakala  6  za mswada wa marekebisho ya katiba, mwenyekiti wa tume hiyo  Wafula Chebukati alisema tume hiyo tayari imebuni kamati itakayoendesha shughuli ya kuthibitisha saini hizo mara tu fedha zitakapopatikana.

Chebukati  alitoa hakikisho kwamba kamati hiyo itakuwa ikitoa habari mara kwa mara kuhusiana na hatua iliopigwa

Makao makuu ya mpango huo wa maridhiano yamesema hayatakubali kushurutishwa na wale wanaoeneza habari za kupotosha kuhusiana na  mpango huo wa  BBI.

Baada ya kupokea saini hizo na kuzithibitisha, mapendekezo kuhusu mswada wa marekebisho ya katiba ya  mwaka 2020  yatakabidhiwa mabunge yote  ya kaunti 47.

Angalau kaunti 24 zinahitajika kuidhinisha mswada huo ili kuiwezesha kuwasilishwa katika bunge la kitaifa.

Kura ya maamuzi inatarajiwa kufanywa kati ya mwezi Aprili na  Juni mwaka wa  2021.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *