Categories
Habari

IEBC yachapisha sahihi za BBI kwa ukaguzi wa umma

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imechapisha orodha ya sahihi zilizobainishwa za mchakoto wa BBI ili ziweze kukaguliwa na umma.

Tume hiyo imechapisha sahihi hizo pamoja na majina kamili ya walioziwasilisha, kaunti zao, maeneo bunge yao na vituo vyao vya kupigia kura.

Hatua hiyo itawezesha wapiga kura kubaini iwapo taarifa zao zilitumika bila idhini yao.

Tume hiyo pia imewahimiza wale ambao watajipata kwenye orodha hiyo lakini hawakuweka sahihi zao wapeleke malalamishi kwa tume hiyo kufikia Jumatatu juma lijalo.

Makarani 400 waliajriwa na IEBC ili kukagua na kuidhinisha sahihi za wapiga kura hao wanaounga mkono mswada unaopendekeza marekebisho ya katiba wa mwaka 2020.

Wiki jana, tume hiyo ilikanusha madai ya Mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohamed kuwa inavuruga shughuli ya kubaini sahihi hizo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *