IEBC: Vitendo vya uhuni havitavumiliwa

Tume ya uchaguzi na mipaka IEBC imesema haitavumilia vitendo vya ghasia huku uchaguzi mdogo wa useneta kaunti ya Machakos ukikaribia.

Tume hiyo ambayo inajiandaa kwa uchaguzi huo utakaoandaliwa tarehe 18 mwezi huu ililaani vikali vitendo vya uhuni na ghasia wakati wa chaguzi ndogo za Alhamisi dhidi ya maafisa wa tume hiyo ambao walikuwa wakitekeleza kazi yao.

Kwenye Taarifa Mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati alisema tume hiyo itaanda warsha ya utoaji ushauri nasaha kwa maafisa wake walipatikana kwenye vurugu za chaguzi ndogo za Alhamisi iliyopita.

Taarifa hiyo imejiri siku mbili baada ya aliyekuwa waziri wa michezo Rashid Echesa kumshambulia afisa wa tume hiyo akiwa kazini wakati wa uchaguzi mdogo wa Matungu.

Katika uchaguzi huo pia afisa mwingine wa tume hiyo alidharauliwa, kusumbuliwa na kisha kushambuliwa kando na kutusiwa na kundi la wahuni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *