Idris Sultan atania Nandy na Koffi

Muigizaji na mchekeshaji wa nchi ta Tanzania Idris Sultan ametania wasanii wa muziki Nandy wa Tanzania na Koffi Olomide wa nchi ya Congo.

Alichukua picha ya pamoja ya wasanii hao wawili na kuandika, “Ni wajibu wetu kama watanzania kuhakikisha tunalinda mali zote za kitanzania na hatuziachi katika hali yoyote hatarishi. UZALENDO sio jambo la kuonea aibu kabisa.”

Anajaribu kutetea Nandy mtanzania mwenzake asije akanyakuliwa na Koffi kuelekea Congo ila ni utani tu kwani picha hiyo walipigwa wakitayarisha video ya wimbo wao ambao utazinduliwa wakati wowote kutoka sasa.

Baadaye Idris alipachika picha yake akisinzia huku ameketi na kuongeza utani dhidi ya Koffi. .

Anasema; “Nimeshtuka usiku baada ya kukumbuka kitu “Koffii si anatoka kwenye source ya vumbi la Congo?” Mungu wanguuuuuu… Narudi kulala”

Vumbi la Congo ni dawa fulani ya kuongeza nguvu za kiume.

Idris Sultan wa umri wa miaka 28 alipata umaarufu nchini Tanzania na Afrika baada ya kushinda shindano la Big Brother mwaka 2014.

Baada ya hapo aliingilia uchekeshaji, uigizaji na utangazaji wa redio ambapo aliongoza kipindi kwa jina, “Mji wa Burudani” kwenye kituo cha redio kiitwacho Choice Fm.

Amewahi kujipata pabaya kutokana na maigizo yake kwenye mitandao ya kijamii kiasi cha kutiwa mbaroni kwa kosa la kuharibia watu jina au kuwaonyesha visivyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *