Categories
Habari

Idadi ya madaktari wanaoaga dunia nchini kutokana na Covid-19 yaongezeka

Daktari mwengine ameaga dunia kutokana na ugonjwa wa Covid-19, huku maafa kutokana na ugonjwa yakiendelea kuongezeka miongoni mwa wahudumu wa afya hapa nchini.

Chama cha madaktari na watalaamu wa meno,KMPDU kimemtambua daktari huyo kuwa Nira Patel ,ambaye alikuwa mtalaamu wa matibabu ya meno.

Kifo chake kimetokea saa kadhaa baada ya mtalaamu wa matibabu ya figo katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta Daktari Anthony Were kuaga dunia,katika hospitali moja jijini Nairobi,ambako alikuwa akipokea matibabu maalumu.

Kikithibitisha kifo chake,chama cha kitaifa cha madaktari na watalaamu wa meno,kilimtaja marehemu kuwa mfanyakazi mwenye juhudi,ambaye alikuwa kielelezo kwa wengi.

Dkt Were alikuwa kinara wa chama cha wataalamu wa tiba za maradhi ya figo na pia naibu mkurugenzi wa taasisi ya utafiti kuhusu ugonjwa wa figo, Kanda ya Afrika Mashariki.

Naibu rais William Ruto ametuma risala ya rambirambi kwa familia,ndugu na marafiki wa marehemu Daktari Anthony Were, ambaye hadi wakati wa kifo chake alikuwa mtalaamu wa matibabu ya figo katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta.

Kupitia kitandazi cha Twitter,naibu rais amesema Marehemu daktari Were alikuwa mtumishi hodari wa umma ambaye alitekeleza majukumu yake kwa njia ya kitalaamu.Hadi sasa wahudumu wengine wa afya 32 wameaga dunia kutokana na ugonjwa huo,huku zaidi ya elfu-20 wakiambukizwa virusi  vya korona.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *