Hellen Obiri kunogesha Kip Keino Classic Jumamosi

Baada ya kusajili muda wa kasi katika mbio za mita 3000 ijumaa iliyopita mjini Doha Qatar ,bingwa wa dunia Hellen Obiri atafunga msimu nyumbani Oktoba 3 atakapotimka mashindano ya Kip Keino Classic Continental tour.

Obiri ambaye tayari ameshiriki mashindano matatu Tangu Agosti mwaka huu, amejumuishwa katika orodha ya wanariadha watakaopambana katika mita 5000 .

Katika  mkondo wa kwanza wa Monaco Obiri alifyatuyka mita 5000 kwa muda wa dakika 14 sekunde 22 nukta 12,lakini akazidiwa maaraifa katika mkondo wa Stockholm Sweeden alipomaliza wa 11 katika mita 1500 na kufunga msimu Doha kwa kusajili  muda wa kasi katika mita 3000 wa dakika  8 sekunde 22 nukta 54.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *