Hatimaye Trump aidhinisha mswaada wa ruzuku kwa waathiriwa wa COVID-19 Marekani

Rais wa Marekani Donald Trump hatimaye ametia saini mswaada wa kuwapa ruzuku waathiriwa wa ugonjwa wa COVID-19.

Awali, Trump alikuwa amekata kutia saini mswada huo na kutaka fungu hilo kuongezwa na kulipwa kwa awamu moja.

Kucheleweshwa kutiwa mswaada huo kunamaanisha kuwa mamilioni ya Wamarekani wasio na ajira walikosa kupata ruzuku zao za kawaida kutoka kwa serikali.

Fungu la ruzuku ya dola bilioni 900 lilikuwa limeidhinishwa na Bunge la Congress baada ya miezi kadhaa ya majadiliano.

Fungu hilo ni sehemu ya jumla ya dola trilioni 2.3 ambazo zinajumuisha kiasi cha dola trilioni 1.4 za matumizi ya kawaida ya serikali.

Laiti Trump hangetia saini mswaada huo, kufikia usiku wa manane wa siku ya Jumatatu, baadhi ya shughuli za serikali zingesimamishwa.

Jambo hilo lingeepukwa tu ikiwa wabunge wangeidhinisha mswaada wa kupata fedha kwa dharura.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *