Hatimaye Aubemeyang asaini kandarasi mpya ya miaka mitatu Arsenal

Kapteni wa kilabu ya Arsenal Pierre Emerick Aubemeyang ametia saini mkataba mpya wa miaka mitatu na timu hiyo  hadi mwaka 2023 .

Kandarasi hiyo mpya itamfanya mshambulizi huyo kutoka Gabon kuwa mwanasoka anayelipwa kitita cha juu Zaidi kwa wiki katika timu hiyo ikiwa pauni 350,000 kila wiki na kumpiku Mesut Ozil.

‘’Hatimaye nimetimiza,nafurahia kusalia hapa,hapa ni nyumbani ,ni siku njema ,nataka kuwa legend wa timu hii na kuacha historia itakayokumbukwa.Ni wakati wa kutia bidii ,nitajitolea kwa kila hali”akasema Aubemeyang  baada ya kumwaga wino kwa karatasi ya kandarasi yake.

Aubameyang alijiunga na Arsenal Januari mwaka  2018 kwa ada ya pauni milioni 56 kutoka  Borussia Dortmund na amefunga mabao  72 katika mechi 112 alizopiga na the gunners.

Yamkini hatua yake ya kusaini kandarasi mpya imetokana na ushawishi mkubwa wa meneja wake Mirkel Arteta.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *