Harmonize achapisha video akiwa na binti yake

Baada ya kufichua kwamba ana mtoto nje ya ndoa, mwanamuziki Harmonize anaonekana kujitolea kutimiza jukumu lake kama babake Zulekha wa mwaka mmoja unusu.

Harmonize ambaye anafahamika pia kama Konde boy aliweka video kwenye mitandao ya kijamii akiwa na binti yake wakiwa nyumbani.

Mwanamuziki huyo hatilii maanani yanayoendelea kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kuvunjika kwa ndoa yake na mwanamke kwa jina Sarah.

Harmonize na binti yake Zulekha

Sarah anashikilia kwamba Konde Boy hana uwezo wa kuzalisha na hivyo huyo mtoto sio wake. Aliweka picha ya majibu ya vipimo vya DNA kwa nia ya kudhibitisha kwamba huyo mtoto sio wa Harmonize.

Harmonize hata hivyo alisema kwamba hawezi kuendelea kumficha mtoto wake kwa aibu ya kumpata nje ya ndoa.

Wakati akitangaza mtoto wake rasmi, alimwomba mkewe msamaha lakini ni kama haukukubaliwa kwani Sarah anazungumza kama ambaye tayari ameacha uhusiano na Harmonize.

Baadaye alishukuru wote ambao wamemsaidia na kumpa maneno ya kumtia moyo huku akikiri upendo wake kwa watanzania kwani Tanzania ni kama nyumbani.

Tetesi kuhusu kutengana kwa waili hao zilizuka mwezi mmoja uliopita lakini zikazimwa na meneja wa Harmonize anayejiita mjerumani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *