Harambee Stars yapanda nafasi mbili msimamo wa FIFA

Timu ya Harambee Stars imepanda kwa nafasi mbili kwenye msimamo wa dunia wa FIFA wa mwezi Machi uliotangazwa Jumatano.

Stars imechupa kutoka nafasi ya 104 duniani hadi ya 102 kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Togo katika mechi ya kufuzu AFCON na kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Misri katika mchuano mwingine.

Kenya ni ya 23 barani Afrika kwa mjibu wa msimamo huo.

Senegal ingali kuongoza Afrika katika nafasi ya 22 ,licha ya kuteremka nafasi 2,ikifuatwa na Tunisia iliyosalia ya 26 wakati Super Eagles ya Nigeria ikikwea nafasi 4 hadi nambari 32 ,wakifuatwa na mabingwa wa Afrika Algeria katika nafasi ya 33.

Atlas Lions ya Moroko ni ya 34 na ya 5 Afrika ,Misri ikapanda nafasi 3 hadi nambari 46,wakifuatwa na Black Stars ya Ghana iliyo ya 49.

Cameroon,Mali na Ivory Coast zinaambatana katika nafasi za 55,57 na 59 katika usanjari huo katika nambari za 8 ,9 na 10 Afrika kwenye usanjari huo.

Uganda Cranes ingali ya kwanza Afrika Mashariki ikiwa ya 84 ikifuatwa na Kenya ,Rwanda na Tanzania katika nafasi za 102,129 na 137 mtawalia.

Nafasi 6 za kwanza ulimwenguni hazibadilika,Ubelgiji,Ufaransa na Brazil zikishikia nafasi za 1,2 na 3 mtawalia.

Uingereza ,Ureno na  Uhispania zimo katika nafasi za 4,5 na 6 kwenye usanjari huo wakati Italia ikipanda kwa nafasi 3 hadi nambari 7,nazo Argentina,Uruguay na Denmark zikiambatana katika nafasi za 8,9 na 10 katika usanjari huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *