Harambee Stars kuanza mazoezi ya kambi Jumatatu

Timu ya taifa harambee stars itaanza mazoezi ya kambi Jumatatu Oktoba 5 kujitayaraisha kwa mchuano wa kirafiki dhidi ya Zambia  Oktoba 9.

Wachezaji 11 waliripoti kwa kambi ya mazoezi Jumapili jioni huku wale wa kigeni wakitarajiwa kuanza kuwasili baadae wiki hii.

Wachezaji na maafisa wa timu hiyo walipitia vipimo vya Covid 19 mmoja baada ya mwingine walipowasili katika kambi Jumapili wka mjibu wa sheria za wizara ya afya na ile ya michezo .

Harambee star imeratibiwa kupimana nguvu na Chipolopolo ya Zambia katika uwanja wa taifa wa Nyao katika mechi hiyo huku wakijiandaa kukabiliana na Comoros katika mechi za nyumbani na ugenini mwezi ujao kufuzu kwa dimba la Afcon mwaka 2021.

Kenya imezoa alama 2 kutokana na mechi mbili za ufunguzi saw ana Misri huku Comoros wakiongoza kwa pointi 4.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *