Categories
Burudani

Hamkutuelewa!!

Wanandoa wawili ambao walijitokeza na kutangaza kwamba wao ni ndugu na pacha sasa wanasema walieleweka visivyo. Hadithi ya wawili hao imeteka mitandao ya kijamii nchini Kenya kwa muda sasa hasa kwa sababu wengi wa wananchi ni wakristo na ndoa kati ya ndugu ni dhambi.

Lakini sasa Brian Chiwera na mke wake Lexy wameelezea kwamba wao sio ndugu wa damu ila wanafanana kama mapacha na kwamba wazazi wao walikuwa marafiki na hivyo walikua pamoja.

Wawili hao wanasema kwamba walilelewa kama ndugu hata kama hawakuwa na uhusiano wa damu na walipopendana, wazazi wao hawakufurahia kwani inasemekana mapenzi kati ya watu wawili ambao wanafanana kabisa kama vile ndugu huleta laana.

Kwa sababu hiyo wanasema wazazi wao waliwakana na kuwatelekeza wakahama nyumbani na kuanza kuishi pamoja na sasa wana mtoto wa kike.
Brian na Lexy walihojiwa kwenye kipindi kimoja cha mitandaoni ambapo walionekana kudinda kufunguka mengi kuhusu maisha yao kwani hata hawakutaka kuzungumzia binti yao.

Kwenye mtandao wa Tik Tok, wawili hao wamekuwa wakiweka picha ambapo wanaonyeshana mapenzi.

Hadithi yao inakanganya na isijulikane kama ni kweli au mambo tu ya kujitafutia umaarufu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *