Categories
Habari

Haji akariri kwamba wahusika wa kashfa ya KEMSA watachukuliwa hatua

Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka ya Umma Noordin Haji amewahakikishia Wakenya kwamba uchunguzi kuhusu kashfa ya KEMSA ungali unaendelea na kwamba waliohusika watashitakiwa.

Haji wakati uo huo amekanusha madai kwamba tume ya maadili na kupambana na ufisadi haitekelezi wajibu wake dhidi ya ufisadi ipasavyo.

Amesema kundi la wataalamu lililobuniwa linakusanya ushahidi kuhusiana na kashfa hiyo.

Haji ameongeza kuwa kuna udhifu kwenye harakati za  kutafuta ukweli kuhusu kashfa hiyo.

Haya yanajiri baada ya malalamishi kutoka kwa viongozi na Wakenya kuhusu kucheleweshwa kwa uchunguzi na kutochukuliwa hatua kwa watu waliotajwa kwenye kashfa hiyo.

Halmashauri ya Usambazaji vifaa vya matibabu nchini KEMSA inakashifiwa kwa kutoa kandarasi za usambazaji wa vifaa hivyo kwa kampuni mbali mbali bila kufuata sheria za kandarasi ipasavyo.

Inadaiwa kwamba kutokana na hayo, Kenya ilipoteza mamilioni ya fedha kiufisadi, fedha zilizonuiwa kusaidia nchi hii katika juhudi za kukabiliana na janga la COVID-19.

Rais Uhuru Kenyatta alikuwa ameagiza uchunguzi ufanywe na wahusika kuchukuliwa hatua za kisheria katika muda wa siku 21, muda ambao uliisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *