GSU na KPA watinga robo fainali mashindano ya voliboli Afrika

Mabingwa wa ligi ya kenya  General Service Unit(GSU)  na Kenya  Ports Authority(KPA) wamejikatia tiketi kwa robo fainali ya mashindano ya klabu bingwa Afrika katika voliboli ya wanaume yanayoendelea mjini Kilibia  Tunisia .

GSU wamesajili ushindi katika mechi ya mwisho ya kundi D Jumanne  baada ya kuwaangusha Espoire  kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Congo seti 30 za  25-11,25-14 na 25-12 .

Ushindi huo unawaweka GSU katika nafasi ya pili kwa pointi 5 baada ya kushinda mechi mbili na kupoteza kwa Zamalek ,huku Zamalek ikiongoza  baada ya kushinda mechi zote tatu za kundi hilo .

Wanabandari KPA wamefuzu kwa robo fainali kwa mara ya kwanza  kufuatia ushindi wa seti 3-0 dhidi ya Rukinzo ya Burundi katika pambano la mwisho la kundi A Jumanne wakisajili ushindi wa  alama 25-23,25-15 na 25-23.

KPA pia wameshinda mechi mbili na kushindwa moja huku wakiibuka wa pili  katika kundi A ,nyuma ya wenyeji Esperance walioshinda mechi zote.

Mashindano hayo yatachukua mapumziko Jumatano  na Alhamisi ,kabla ya kuingia kwota fainali kuanza Ijumaa  GSU wakiwa na miadi dhidi ya Esperance .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *