Categories
Michezo

Gor wazidi kutota ligini baada ya kushindwa na Posta Rangers

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Kenya Gor Mahia waliendeleza msururu wa matokeo duni ligini baada ya kuambulia kichapo cha pili mtawalia walipolazwa na Posta Rangers bao 1-0 katika mojawapo wa mchuano wa ligi uliosakatwa katika uwanja wa Kasarani Jumatano alasiri.

Kiungo Francis Nambute alipachika bao la pekee la ushindi kwa Rangers dakika ya kwanza ya ziada katika kipindi cha kwanza, huku Kogalo wakipoteza nafasi  nyingi za kusawazisha  hadi kipenga cha mwisho.

Ilikuwa mechi ya pili mtawalia kwa Gor kupoteza na ya sita msimu huu baada ya ksuhindwa na  KCB mabao 2-0 mwishoni mwa juma lililopita.

Gor Mahia ingali ya 8 ligini kwa pointi 19  na watarejea uwanjano Machi 21 dhidi ya Bidco United.

Rangers kwa upande wao wamepanda hadi nafasi ya 14 kwa alama 14 kufuatia ushindi huo.

Katika pambano jingine la Jumatano Zoo Fc ya Kericho na Western Stima walitoka sare tasa katika uwanja wa Kericho Green.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *