Gor waanza vyema msimu huku Ingwe wakidumisha rekodi ya asimilia 100%

Mabingwa wa ligi kuu ya soka humu nchini Gor Mahia walianza kampeini za kutetea taji yao ya ligi kwa ushindi baada ya kuifunga Ulinzi Stars bao 1-0 katika mechi iliyochezwa katika uwanja wa taifa wa Nyayo hapa Nairobi siku ya Jumamosi.

Mechi hiyo ambayo pia ilikuwa ya kuadhimisha sikukuu ya Jamhuri ilikuwa ya kwanza msimu huu kwa timu hizo mbili huku Jules Ulimwengu wa Burundi akipachika bao hilo muhimu kwa kogalo katika dakika ya 65.                               

Kwenye mechi nyingine zilizochezwa leo Kariobangi Sharks ilitoka sare kwa kufungana mabao 2-2 na Bidco United ilihali Tusker FC iliifunga Western Stima mabao 5-2 huku  AFC Leopards wakidumisha rekodi ya asilimia 100 kwa kuipakata Sofapaka mwabao 3-0 yote yakifungwa na Elvis Rupia .

Ligi hiyo kuendelea Jumapili , Vihiga United  ikichuana na Nzoia Sugar  ilihali Posta Rangers itacheza na Wazito FC.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *