Gor Roberto Oliveira Goncalves do Carmo kuteuliwa kuwa kocha mpya wa Gor Mahia
Gor Mahia wanatarajiwa kumteua kocha mpya kujaza nafasi ya Steve Polack aliyejiuzulu.
Kwa mjibu wa taarifa kutoka Afisi ya Gor, Roberto Oliveira Goncalves do Carmo atateuliwa kuwa kocha mpya wa timu hiyo kesho siku kadhaa baada ya kujiuzulu kwa Mwingereza Steven Polack kwa maafikiano.
Oliveira ambaye ni raia Brazil mawenye umri wa miaka 60 alikuwa mshambulizi wa zamani wa Brazil akifahamika kama Robertinho, na ana tajriba ya miaka 15 barani Afrika akihudumu katika mataifa ya Tunisia, Angola na hivi punde akiwa na Rayon Sports ya Rwanda.
Kulingana na katibu mkuu wa Gor Mahia Sam Ochola walihiria kumrteua Mbrazil huyo baada ya juhudi za kumpata José Marcelo Ferreira kugonga mwamba.