Gor Mahia wazima Stima Kisumu
Mabingwa watetezi Gor Mahia wameiteketeza Western Stima mabao 3-1 katika mechi ya ligi kuu FKF Jumatatu alasiri katika uwanja Moi kaunti ya Kisumu .
Sammy Onyango alifungua ukurasa kwa bao la dakika ya 23 kabla ya Godfrey Villa Orachaman kuwarejesha wenyeji mchezoni kwa bao la dakika ya 38 huku kipindi cha kwanza kikimalizika kwa sare ya bao 1-1.
Tito Okello kutoka Sudan Kusini aliwahakikisha Kogalo ushindi kwa mabao ya dakika za 65 na 88 ukiwa ushindi wa tatu kwa Gor msimu huu baada ya kusakata mechi 5 ,wakishikilia nafasi ya 8 kwa pointi 9.
Katika mchuano mwingine vijana wa Mathare United wameipakata Zoo Fc mabao 2-0 .
KCB wangali kuongoza kwa alama 18 kutokana na mechi 7 wakifuatwa na Tusker Fc kwa pointi 17 huku Kariobangi Sharks ikiwa ya tatu kwa alama 15.