Gor Mahia waponzwa na kisomo ‘haba’ cha kocha Robertinho

Mabingwa wa ligi kuu ya Kenya Gor Mahia watazikosa huduma za kocha wao  Roberto Oliveira kwa mechi zote za ligi ya mabingwa Afrika msimu huu baada ya kufungiwa na shirikisho la soka Caf.

Kulingana na Caf ,kocha anayesimamia kilabu kinachosriki michuano ya ligi ya mabingwa ,lazima awe na leseni ya Caf A ,Uefa Pro au Pro kutoka mashirikisho mengine ya soka huku raia huyo wa Brazil akiwa na na leseni ya B kutoka nchini kwao Brazil ambayo ni sawa na leseni ya Caf  C

Hatua hii ina maana kuwa kocha huyo aliye na umri wa miaka 60  hataruhusiwa kuwa uwanjani wakati Gor Mahia itakapochuana na APR ya Rwanda Novemba 28  na pia pambano la marudio hapa Nairobi wiki moja baadae.

Uamuzi huo unaicha Kogalo kwenye njia panda ambapo itawalazimu kumtafuta kocha mpya wa msimu huu au kocha mpya aliyehitimu kwa mechi zao za ligi ya mabingwa Afrika.

Robertinho alishika hatamu za kuwanoa Gor kutoka Steven Polack aliyejiuzulu.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *