Miamba wa soka nchini Gor Mahia wanalenga kufuzu kwa hatua ya makundi ya kombe la ligi ya mabingwa barani Afrika Caf kwa mara ya kwanza msimu huu.
Kulingana na meneja wa Gor Jolawi Obondo kikosi walicho nacho kwa sasa ni kizuri na pia kina tajriba ya kuweka rekodi kuwa kilabu cha kwanza kutoka humu nchini kucheza hadi hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa baada ya majaribio kadhaa bila ufanisi.
“Ni maombi yetu tucheze hadi hatua ya makundi na hata ikiwezekana hadi hatua ya mwondoano ya ligi ya mabingwa barani Afrika”akasema Obondo
Kwa mjibu wa Obondo Kogalo pia ina fursa ya kwenda mbali msimu huu katika kombe hilo kutokana na usaidizi wanaopata kutoka kwa Wizara ya michezo na shirikisho la FKF na kukanusha madai kuwa kikosi cha sasa ni hafifu na hakina uwezo wa kwenda mbali..
“Watu wanasema huenda hatuna kikosi kizuri lakini mimi sikubaliani,tuna kikosi kizuri na tuko na usaidizi kutoka kwa serikali,wizara na hata shirikisho sioni kwa nini tushindwe kufika hatua ya makundi” akaongeza Obondo
“Ushindi unataegemea na mtazamo,malengo na pia ushirikiano wa wachezaji ,usaidizi wa na maono ya kocha na nadhani tumejianda kwa hayo yote”akasema Obondo
Nahodha wa kilabu hicho Keneth Muguna pia anaazimia kuingoza Kogalo hadi hatua ya makundi licha ya upinzani mkali watakaopata.
“Tunataka tufuzu ,na kila timu pia inataka kufuzu ,tunajua itakuwa ngumu lakini mwisho wa siku sisi tunajua sisi ndio tutashinda na kufuzu hatua ya makundi ya Caf Champions League”akasema Muguna
Gor Mahia imeratibiwa kuchuana na mabingwa wa Algeria CR Belouizdad ya Algeria tarehe 22 mwezi huu mjini Algiers kabla ya kuwaalika wageni hao tarehe 5 mwezi ujao kisha mshindi kijumla afuzu kwa hatua ya makundi ya kombe la ligi ya mabingwa Afrika.
Mabingwa hao mara 18 wa ligi ya Kenya walifuzu kwa raundi ya pili ya mchujo wiki jana baada ya kuibandua APR ya Rwanda mabao 4-3 kwa jumla katika raundi ya kwanza ya mchujo.
Kogallo wamekuwa wakibanduliwa katika hatua ya mchujo ya ligi ya mabingwa Afrika kwa misimu mitatu mtawalia iliyopita,baadae wakafuzu kwa hatua ya makundi ya kombe la shirikisho .
Hata hivyo Gor wameshindwa kuingia hatua ya mwondoano ya kombe la shirkisho katika misimu mitatu iliyopita.
Mabingwa hao mara 18 wa ligi ya Kenya walifuzu kwa raundi ya pili ya mchujo wiki jana baada ya kuibandua APR ya Rwanda mabao 4-3 kwa jumla katika raundi ya kwanza ya mchujo.