Gor Mahia wako ngangari kumenaya na APR Jumamosi

Mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini Gor Mahia wanaendelea na maandalizi kwa mechi ya marudio awamu ya mchujo kuwania taji la ligi ya mabingwa Afrika Caf  jumamosi hii  dhidi ya APR ya Rwanda katika uwanja wa taifa wa Nyayo kuanzia saa kumi alasiri.

Gor Mahia ukipenda Kogalo wanahitaji ushindi wa bao 1-0 Jumamosi jioni ili kutinga mchujo wa pili baada ya kushindwa mabao 1-2 katika mkumbo wa kwanza Jumamosi iliyopita mjini Kigali Rwanda na wanajeshi hao wa APR.

Kogalo wanawinda ushindi huo muhimu ili kujikatia tiketi kwa mchujo wa pili ambapo wameratibiwa kupambana na mshindi kati ya Al Nasr kutoka Libya dhidi ya mabingwa wa Algeria CR Belouizdad .

Belouizdad walipata ushindi wa mabao 2-0  dhidi ya Al Nasr katika mkumbo wa kwanza huku mechi ya marudio ikisakatwa Ijumaa hii.

Gor wanalenga kufuzu kwa hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa kwa mara ya kwanza baada ya kubanduliwa katika mchujo kila mwaka walioshiriki kombe hilo huku walikazimika  kugura katika hatua ya makundi ya kombe la shirikisho .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *