Gor kukabiliana na mabingwa wa Algeria Belouizdad

Mabingwa wa ligi kuu ya Kenya Gor Mahia wameratibiwa kuchuana na mabinwga wa Algeria CR Belouizdad  katika mchujo wa pili wa ligi ya mabingwa barani Afrika Caf  Disemba 22 mjini Algiers huku pambano  la marudio likichezwa Nairobi Janauri 5 mwaka ujao.

Gor walitinga hatua hiyo baada ya kuishinda Rwanda Patriotic Army mabao 3-1 Jumamosi iliyopita katika uwanja wa Nyayo na kufuzu kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-3 .

Upande wao Beloiuzdad waliishinda  Al Nasr ya Libya magoli 2-0 Jumapili jioni na kufuzu kwa hatua ya mchujo wa pili kwa ushindi wa jumla wa magoli 4-0.

Kogalo wamekuwa na rekodi mbovu wanapocheza ugenini dhidi ya vilabu vya  Algeria baada ya kucharazwa mabao 4-1 na Usm Algers mwaka uliopita mjini Algiers katika hatua ya mchujo wa ligi ya mabingwa kabla ya kupoteza bao moja kwa bila ugenini dhidi ya Na Hussein Dey katika hatua ya makundi ya kombe la shirikisho la soka .

CR Belouizdad

Ili kuwa na matumaini ya kufuzu kwa hatua ya mwisho ya mchujo ni lazima  Gor warekebishe makosa kadhaa haswa ya safu ya ulinzi na pia kujipanga mapema na kusafiri kwa wakati ufaao.

Mshindi wa mchuano kati ya Gor na Belouizdad atacheza  mchujo wa mwisho itakayompa fursa mshindi kuingia hatua ya makundi ya kombe la  ligi ya mabingwa .

Belouizdad wamenyakua taji ya ligi kuu Algeria mara 7 na kombe la shirikisho nchini Algeria mara 8 na ni miongoni mwa timu zilizo na ufanisi mkubwa nchini humo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *