GEMA yamuidhinisha Mutua Katuku kuwania Useneta wa Machakos

Kundi la Muungano wa jamii za eneo la mlima Kenya almaarufu Gema limemuidhinisha mgombeaji wa chama cha Maendeleo Chap Chap kwa kiti cha useneta, kaunti ya Machakos Mutua Katuku.

Kundi hilo wakiwemo wafanyabiashara na wazee waliandaa tambiko la kumtawaza Katuku.

Hafla hiyo iliyoandaliwa katika uwanja wa maonyesho ya kilimo wa Machakos ilisimamishwa na mwenyekiti wa jamii ya Gema katika kaunti ya Machakos, Joseph Githehu.

Katuku alisindikizwa kwenye hafla hiyo na maafisa wakuu wa chama cha Maendeleo Chap Chap wakiongozwa na aliyekuwa spika wa bunge la kaunti ya Machakos, Bernard Mungata.

Kinyang’anyiro cha uchaguzi huo mdogo ambao umepangiwa kuandaliwa tarehe 18 mwezi Machi kimevutia zaidi ya wagombeaji kumi.

Viongozi wa ngazi za juu kutoka chama cha Wiper kinachoongozwa na Kalonzo Musyoka, chama cha Maendeleo Chap Chap cha gavana Alfred Mutua na kile cha United Democratic Alliance wameimarisha kampeni kabla ya uchaguzi huo mdogo.

Miongoni mwa wagombeaji wa kitti hicho ni Agnes Kavindu Muthama wa chama cha Wiper, Ulbanus Ngengele wa UDA na Mutua Katuku wa Maendeleo Chap Chap.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *