Gavana Muriithi atoa wito wa mjadala wa kuboresha ripoti ya BBI

Gavana wa Kaunti ya Laikipia Ndiritu Muriithi ametoa wito wa mjadala wa kuboresha ripoti ya mpango wa maridhiano wa kitaifa, BBI.

Muriithi amesema viongozi wanafaa kufahamu kuwa utayarishaji wa katiba ni mchakato wa muda mrefu, kwa hivyo ipo haja ya mjadala wa manufaa kuhusu ripoti hiyo ili kuiboresha.

“Tujadiliane tulete mawazo ambayo yanaweza kuendesha Kenya mbele. Isiwe kila saa ni matusi ambayo hayana maana,” amesema Muriithi.

Muriithi, aliyekuwa akiongea mjini Nyahururu amesema ripoti hiyo ina mapendekezo yanayostahili lakini inafaa kuboreshwa ili kuimarisha ugatuzi kwa kupandisha hadhi ya Bunge la Seneti miongoni mwa masuala mengine.

Amesema magavana ni sharti wahakikishe kuwa mapendekezo yanayohusiana na nyongeza ya pesa kwa maeneo ya kaunti yamekitwa kwenye ripoti hiyo.

Gavana huyo amesema suala la kuchelewa kutoa pesa kwa maeneo ya kaunti sharti lishughulikiwe na BBI.

Baraza la Magavana limependekeza marekenbisho makubwa yapatayo matano kwenye ripoti hiyo ya BBI.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *