Flamengo wanyakua taji ya 7 ya ligi kuu Brazil serie A

Klabu ya Flamengo imehifadhi taji ya ligi kuu nchini Brazil maarufu Serie A licha ya kucharazwa mabao 1-2 ugenini na Sao Paulo katika mechi ya kufunga msimu mapema Ijumaa.

Wapinzani wa Flamengo ,Internacional walihitaji kuwashinda Corrinthians wakiwa nyumbani katika mechi ya kumaliza msimu lakini wakaambulia sare tasa.

Flamengo imetawazwa mabingwa kwa msimu wa pili mtawalia baada ya kuzoa pointi 71,alama moja zaidi ya Internacional.

Timu za Vasco Da Gama,Goias,Coritiba na Botafofob zimeshushwa daraja hadi Serie B.

Flamengo wameshinda taji ya Serie A kwa amara ya 7 na kushinda mara mbili mtawalia kwa mara ya kwanza tangu Zico kufanya hivyo akiwa mkufunzi wa timu hiyo mwaka 1982 na 1983.

Vilabu vinne vya Flamengo,Internacional,Atletico MG na Sao Paulo zimefuzu kushiriki mashindano ya kombe la Copa Libertadores ambayo ni sawa na EUFA Champions League.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *