FKF yaongeza muda wa uhamisho wachezaji

Shirikisho la kandanda nchini limeongeza muda wa usajili na uhamisho wa wachezaji kutoka siku ya mwisho Novemba  2  hadi Novemba 6 .

Kulingana na Fkf   muda wa usajili na uhamisho kwa vilabu vinavocheza mechi za mchujo  kuingia ligi kuu ya Fkf umeongezwa hadi Novemba 13.

Hata hivyo uhamisho wa wachezaji wa kigeni kuingia humu nchini  ulifungwa Jumatatu Novemba 2 .

Ligi kuu ya Fkf itang’oa nanga  Novemba 21 huku ligi nyingine za NSL,Division one,ligi kuu ya wanawake zikitarajiwa kuanza mwaka ujao.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *