Categories
Michezo

FIFA yapiga marufuku mashirikisho ya soka ya Chad na Pakistan

Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA limepiga marufuku shirikisho la kandanda nchini Pakistan na chama cha soka nchini Chad kutokana na mwingilio wa serikali .

Baraza kuu la FIFA liliafikiana kw akauli moja kupiga marufuku chama cha soka nchini Chad FTFA,baada ya serikali kuvunjilia mbali chama hicho na kuunda kamati ya muda kuendesha soka  kinyume na sheria za FIFA.

Hatua hiyo ilichangia CAF kuipiga marufuku timu ya Chad katika mechi mbili za mwisho za makundi kufuzu kwa kombe la AFCON mwaka ujao.

Pia baraza la FIFA limefungia shirikisho la kandanda nchini Palistan PFF pia kutokana na mwingilio wa watu kwenye usimamizi wa kandanda.

Yamkini kulikuwa na maandamano kwenye kamao makuu ya PFF huku kamati ya muda inayoongozwa na Haroon Malik  iliyoundwa na FIFA iking’atuliwa afisini na uongozi kukabidhiwa kwa  Syed Ashfaq Hussain Shah.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *