Faith Chepng’etich atamba Ostrava Golden Spike

Bingwa wa  Olimpiki Faith  Chepng’etich alitwaa ushindi  katika mbio za mita 1500 kwenye mashindano  ya Ostrava Golden Spike jana usiku Jamhuri ya  Czech.

Huo ulikiwa mkondo wa tano wa mashidnano ya world continental tour nembo ya dhahabu.                                                                                        

Kipyegon aliziparakasa mbio  hizo huku  akiweka  rekodi  mpya  ya mkondo   ya dakika 3 sekunde  59 nukta 5.

Mwingereza Laura  Weigthman aliibuka Wa pili kwa  dakika 4 sekunde 1   nukta  96, huku Jemma Reekie wa Uingereza akitwaa  nafasi ya tatu.

Katika matokeo mengine ya  jana usiku bingwa wa Ulaya  Jakob Ingebristen kutoka Norway ,aliibuka mshindi katika miat 1500 kwa dakika 3 sekunde 33 nukta 92 ,akifuatwa na Mkenya Kumari Taki aliyeandikisha muda wake bora wa , huku StewartMcSweyn wa Australia akiambulia nafasi ya tatu.

Chipukizi wa Uganda Jacob Kiplimo aliandikisha rekodi ya mashindano ya golden spike katika mita 5000 alipozikamilisha kwa dakika 12 sekunde 48 nukta 63,akifuatwa na Selemon Barega wa Ethiopia kwa dakika 12 sekunde 49 nukta 08, naye Yemaneberhan Crippa wa Italia akitwaa nafasi ya tatu kwa dakika 13 sekunde 2 nukta 26.

Sheila Chelengat wa Kenya alimaliza wa  pili kwenye mbio za mita 5000 akichukua dakika 14 sekunde 40 nukta 51 ukiwa muda wake bora ,nyuma ya Sifan Hassan wa Uholanzi aliyetwaa ushindi kwa dakika 14  sekunde  37 nukta 85 ,wakati Yasmin Can wa Uturukia akiridhia nafasi ya tatu.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *