Fahamu viwanja 4 vitakavyotumika kuandaa michuano ya CHAN nchini Cameroon
Makala ya 6 ya fainali za kuwania kombe la CHAN yataandaliwa katika viwanja vinne vilivyo katika miji mitatu nchini Cameroon baina ya Januari 16 na Februari 7 mwaka huu.
Uwanja wa Ahmadou Ahidjo ni uga wa michezo yote na ulijengwa mwaka 1972 mjini Younde na ulifanyiwa ukarabati mwaka 2016 ili kuandaa fainali za kombe la Afcon kwa wanawake .
Timu ya taifa ya Cameroon huchezea mechi zake katika uga huo ulio na uwezo wa kumudu mashabiki wapatao 40,000 na utaandaa mechi 5 za Kundi A na moja ya kundi B ,robo fainali moja na fainali .

Japoma au pia unafahamika kama Omnisport de Doula ni uga unaopatikana katika mji wa Douala na unamudu mashabiki 50,000 na uligharimu dola milioni 143 kujenga na pia utatumika kuansdaa mechi za kombe la Afcon mwaka ujao.
Uchanjaa huu utaandaa mechi 5 za kundi B na moja ya kundi A ,mchuano mmoja wa robo fainali na mmoja wa nusu fainali.

Stade De la Reunification Doula ni uwanja unaomilikiwa na shirikisho la soka nchini Camerooon na unaselehi mashabiki 30,000 na ulijengwa mwaka 1970 kabla ya kukarabatiwa mwaka 2018.
Uchanjaa huu utatumika kwa mechi 5 za kundi C,mmoja wa kundi D ,mmoja wa robo fainali na mechi ya kuwania nafasi ya tatu na nne.
Limbe Omnisport ni uwanja unaopatikana katika mji wa Limbe na unamudu mashabiki 20,000.
Uga huu ulijengwa mwaka 2012 na kufunguliwa rasmi mwaka 2016 ,na unamilikiwa na shirikisho la soka nchini Cameroon .

uwanja wa Limbe utaanda mechi 5 za kundi D mmoja wa kundi C ,robo fainali moja na nusu fainali moja.
Fainali za 6 za Chan zitang’oa nanga Jumamosi hii Januari 16 huku mechi zote 32 zikipeperushwa kupitia runinga ya taifa KBC Channel one.