Categories
Habari

Evans Kidero aambukizwa Covid-19 wiki moja baada ya kuchanjwa dhidi ya virusi hivyo

Aliyekuwa gavana wa kaunti ya Nairobi  Evans Kidero amepatikana kuwa na virusi vya corona wiki moja baada ya kupewa chanjo dhidi ya maradhi hayo ya  Covid-19.

Kidero alidhibitisha siku ya jumatano asubuhi kupitia ukarasa wake wa facebook kuwa alipatikana na virusi hivyo.

Kidero alisema kuwa alipimwa siku ya jumanne tarehe 6 mwezi huu pamoja na familia yake baada ya kuonyesha dalili za ugonjwa wa Covid-19.

Alisema kuwa baada ya kuchanjwa wiki iliyopita, alipata dalili za Covid-19 na akaamua kwenda kupimwa pamoja na familia yake.

Matokeo yalitolewa Jumatano na akagundua kuwa yeye tu ndiye aliyekuwa ameambukizwa virusi hivyo huku akisema kuwa atajitenga kwa wiki mbili.

Rekodi za hivi punde za wizara ya afya zinaonyesha kuwa wakenya wapatao elfu 370 wamepewa chanjo hiyo dhidi ya ugonjwa wa  COVID-19, huku kaunti ya Lamu ikiandikisha idadi ya chini ya watu waliochanjwa ya watu 262.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe alisema kuwa watu wapatao 277 wameathiriwa vibaya na chanjo hiyo kote nchini.

Baadhi ya athari zinajumuisha kuumwa na kichwa miongoni mwa maumivu mengine.

Hata hivyo maumivu haya yamesemekana kutulia baada ya muda wa siku mbili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *