Ethiopia yakanusha kuwashambulia raia katika jimbo la Tigray

Maafisa wa serikali kuu ya Ethiopia wamekanusha ripoti kwamba raia walilengwa kwenye mashambulizi ya angani katika mji mkuu wa eneo la Tigray.

Walisema operesheni hiyo ililenga vituo muhimu vya kundi la “Tigray People’s Liberation Front” -(TPLF).

Shambulizi moja la angani siku ya Jumanne lilisababisah vifo vya watu wawili na kuwajeruhi wengine kadhaa katika mji huo wa Mekelle.  Haijabainika ni nani aliyetekeleza shambulizi hilo.

Hayo yanajiri baada ya majeshi ya  Ethiopia kuteka miji miwili kaskazini mwa Tigray, ambako wapiganaji watiifu kwa kundi la (TPLF) wanapambana na serikali kuu.

Kiongozi wa Tigray amedhibitisha kutekwa kwa miji hiyo lakini akaongeza kwamba hiyo ni hasara ya muda mfupi huku akiapa kuishinda serikali.

Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed anasema majeshi yake yameukaribia mji mkuu katika eneo la Tigray Mekelle.

Ma-mia ya watu wameripotiwa kuuawa katika mapigano hayo ya majuma mawili.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *