Empoli FC yarejea ligi kuu Italia Serie A baada ya misimu miwili

Klabu ya Empoli  imerejea katika ligi kuu Italia Serie A baada ya kuwa nje kwa misimu miwili kufuatia ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya klabu ya  Cosenza  katika mechi ya ligi ya daraja ya kwanza maarufu kama serie B.

Ushindi huo wa Jumanne unamaainisha kuwa  Empoli wamepandishwa  hadi ligi kuu zikisalia mechi mbili msimu ukamilike  wakizoa pointi 70,alama 7 zaidi ya wapinzani wao wa karibu  Salernitana walio kwenye nafasi ya pili,Lecce na Montana zilizo na alama sawa 61.

Ni mara ya  5 kwa Empoli inayofunzwa na kocha mwenye umri mdogo Alessio Dionisi  kupandishwa daraja hadi ligi kuu Serie A katika kipindi cha miaka 20 iliyopita .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *