Elly Ajowi atuzwa mwanaspoti bora wa SJAK mwezi Machi

Bondia Elly Ajowi ametawazwa mwanaspoti bora wa mwezi Machi katika tuzo za kila mwezi za chama cha wanahabari wa michezo nchini SJAK siku ya Jumatano.

Ajowi ambaye ni Koplo katika kikosi cha taifa cha Polisi amepokea tuzo hiyo ya LG/SJAK baada ya kunyakua dhahabu ya uzani wa heavy kwenye mashindano ya Africa zone 3  yaliyoandaliwa mjini Kinsasha DR Congo mwezi jana .

Kwenye mashindano hayo ,Ajowi ambaye pia amefuzu kwa michezo ya olimpiki mwaka huu , alimshinda  bingwa wa afrika Maxime  Yegnong wa Cameroon kwenye fainali ya uzani wa super heavy .

“Nahisi vizuri kuteuliwa kuwa mshindi wa tuzo ya mwanaspoti bora wa mwezi.Hii inanimotisha zaidi kuleka makuu mwaka huu “akasema Ajowi

Ajowi akipokea tuzo kutoka kwa meneja wa mauzo na mawasiliamo wa LG Maureen Kemunto

Ajowi aliwashinda wapinzani watatu wakiwemo  Wilson Bii wa riadha kwa walemavu, Rakep Patel wa cricket na
Victor Obiero wa  kabaddi.

Meneja mkurugenzi wa  LG  Sa Nyoung Kim amempongeza  Ajowi kwa matokeo yake bora katika Jamhuri ya demokrasia ya Congo  DR Congo.
“Ningependa kumpongeza  Elly Ajowi kwa matokeo yake mazuri ,tunamsherehekea na kumtakia mema anapoelekea michezo ya Olimpiki  mwaka huu”akasema Kim.

Kwa upande Rais wa chama cha waandishi habari za michezo nchini SJAK ,Chris Mbaisi amesema ushirikiano huo kati ya chama hicho na  kampuni ya LG ambao utasaidia kuwatambua na kuwatuza wanamichezo bora nchini.

“Kuwatambua wanamichezo ni njia bora ya kuwashukuru matokeo ya wakenya katika michezo”akasema Mbaisi

Ajowi alipokea runinga ya inchi 55 na tuzo kwa ushindi huo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *